Klabu ya UD Songo imepanga muda wa mchezo wa kesho wa ligi ya mabingwa hatua ya awali dhidi ya Simba utapigwa saa tisa Alasiri kwa muda wa Msumbiji ambao huku Tanzania itakuwa saa kumi jioni
Kikosi cha Simba kiliondoka nchini mapema leo kuelekea Msumbiji tayari kwa mchezo huo
Msafara wa Simba ulijumuisha wachezaji 19 ambao watarejea kesho baada ya mchezo
Mabingwa hao wa Tanzania bara, wana kazi moja tu ya kupata matokeo ya ushindi au hata hata sare ugenini ili kujiweka katika nafasi nzuri mchezo wa marudiano utakaopigwa uwanja wa Taifa
Simba inapewa nafasi kubwa ya kufuzu raundi ya kwanza kutokana na uimara wa kikosi chake, hata hivyo matokeo mazuri kwenye mchezo huo wa ugenini ni muhimu
UD Songo sio timu ya kubeza,Β imekuwa na takwimu nzuri inapocheza katika uwanja wake wa nyumbani
cutHata hivyo, msimu uliopita iliondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na Nkana Fc kwa kufungwa 2-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani na kisha kuchapwa 1-0 mchezo wa marudiano uliuopigwa Zambia
Nkana Fc ilikutana na kipigo cha Simba na kuondoshwa kwenye michuano hiyo baadae
Msimu wa 2017/18 UD Songo ndio ilipata mafanikio zaidi kwa kufanikiwa kuiondosha Al Hilal na baadae kuifunga TP Mazembe kwenye mchezo wake wa nyumbani
Baada ya mchezo wa kesho, timu hizo zitarudiana kati ya August 23-25 katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Taifa, mbele ya maelfu ya mashabiki wa Simba