Simba Day yamuongezea mzuka Kahata

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Aug 2019
Simba Day yamuongezea mzuka Kahata

Baada ya kushuhudia 'nyomi ya kufa mtu' Uwanja wa Taifa wakati wakiibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Power Dynamsos ya Zambia, kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Mkenya Francis Kahata, amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuisapoti timu yao ili iendelee kufanya makubwa zaidi.

Mashabiki wa Simba, Jumanne wiki hii walijitokeza kwa wingi na kufanikiwa kuujaza Uwanja wa Taifa huku wengine wakilazimika kuwekewa TV katika Uwanja wa Uhuru ili kushuhudia kilichokuwa kikiendelea siku hiyo ya kilele cha Simba Day, ambayo waliitumia kutangaza nyota wao wa msimu mpya pamoja na kucheza mechi hiyo ya kirafiki.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kahata alisema anaamini kutokana na ubora wa wachezaji wanaounda kikosi hicho, wanaweza kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa na kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Bara.

"Kinachotakiwa ni kuendelea kushirikiana na kucheza kitimu, pia mashabiki wasichoke kutuunga mkono ili kutupa hamasa ya kufanya vizuri zaidi katika mechi zetu kama walivyofanya Simba Day," alisema.

Kahata ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea Gor Mahia, wakati akiitumikia timu hiyo ya Kenya akiwa na Mnyarwanda Meddie Kagere, walitengeneza ushirikiano mzuri na kuifanya safu yao ya ushambuliaji kuwa tishio na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Kenya.

Na kwa muda mrefu, Kagere alikuwa akitamani nyota huyo kusajiliwa Simba ili waweze kuendeleza ushirikiano wao wa kucheka na nyavu, jambo ambalo mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi hao wanasubiri kuliona likitokea.

Simba ambayo msimu uliopita ilifika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf), imeondoka leo asubuhi kwa ndege ya kukodi kuelekea Msumbiji tayari kwa kuanza kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi kwa kuivaa UD Songo kwenye mechi ya raundi ya awali.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’