Jumamosi ya August 10 2019, kikosi cha Simba kitakuwa nchini Msumbiji kumenyana na UD Songo kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa, hatua ya awali
Afisa Mtendaji Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Crescentius Magori, amesema timu itaondoka keshokutwa Ijumaa kwa usafiri wa ndege na kukodi
"Timu itaondoka Ijumaa asubuhi kuelekea Msumbiji kwa ndege ya kukodi na tutarejea baada ya mechi kumalizika kuja kujiandaa na mechi ya marudiano pamoja na ile ya ngao ya Jamii dhidi ya Azam," amesema
"Tumefanya hivyo ili kukwepa usumbufu wa kuunganisha ndege mbili kwa wakati mmoja ilihali tunaweza kufanya mambo makubwa kwa ajili ya klabu yetu"
Simba itacheza na Azam FC August 17 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii
ADVERTISE HERE