Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wamewapa furaha maelfu ya mashabiki wao waliofurika uwanja wa Taifa baada ya kuichapa Power Dynamo mabao 3-1 katika mchezo wa kuhitimisha maadhimisho ya Sportpesa Simba Week
Mchezo huo ulipigwa baada ya shamrashamra za utambulisho wa kikosi cha Simba uliofanywa na "De Le Boss" Haji Manara
Meddie Kagere 'Terminator' ndiye aliyeinogesha siku ya leo baada ya kufunga hat-trik
Kagere alipachika mabao ya Simba katika dakika za 3', 58' na 73'


Huu ni mwanzo mzuri kwa kikosi kipya cha Patrick Aussems ambacho mwishoni mwa wiki kinakabiliwa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo
Aidha, mashabiki wa Simba leo wameweka rekodi nyingine baada ya kuujaza uwanja wa Taifa huku umati wa mashabiki ukibaki nje baada ya uwanja huo unaochukua mashabiki 60,000 kujaa

Moja ya matukio ya kuvutia leo ni tukio la Mwekezaji Mohammed Dewji 'Mo' kuvaa kama mchezaji kisha kujichanganya na wachezaji uwanjani kwa muda mfupi na baadae kwenda kukaa jukwaani
Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ambaye ni Mwana Simba damudamu leo alishuhudia mchezo huo akiwa amekaa kwenye benchi la wachezaji