Idadi kubwa ya mashabiki wa Simba wameendelea kumiminika kwenye uwanja wa Taifa tayari kwa tukio la utambulisho wa kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania Bara
Mpaka muda huu tiketi za Tsh 5,000/- zimemalizika hivyo kwa wale ambao hajakuwa wamekata, watalazimika kulipia za 15,000/- au 30,000/-
Tayari shamrashamra zimeanza ambapo Simba Queens ilifungua sherehe za leo kwa kuumana na timu ya JKP na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Shuguli rasmi ya utambulisho inatarajiwa kuanza saa 11 na nusu jioni
ADVERTISE HERE