Sisi ni kawaida yetu kuujaza uwanja wa Taifa - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Aug 2019
Sisi ni kawaida yetu kuujaza uwanja wa Taifa - Manara

Mkuu wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amesema leo ni siku nyingine kwa Wanasimba kuandika historia katika hafla ya kilele cha wiki ya Sportpesa Simba Week inayofanyika uwanja wa Taifa

Manara amesema anafahamu mashabiki wa Simba wanaipenda sana timu yao na ndio maana ni kawaida yao kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa Simba inapofanya matukio muhimu

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Manara alisema leo wanakwenda kuandika historia nyingine katika siku maalum ya utambulisho wa timu yao

"Tunajua kesho(leo) ni siku ya kazi lakini kwa Simba haijalishi, nakumbuka mara ya mwisho tulikuwa tunacheza na Al Ahly siku ya Jumanne kama ya kesho (leo) tena tulikuwa tumetoka kufungwa mechi mbili mfululizo kwa goli tano tano lakini bado wanasimba wakaujaza uwanja kiasi cha kuwashangaza Ahly," amesema

"Kwa hiyo naamini kwa kesho (leo) pamoja na kuwa ni siku ya kazi, utambulisho wa wachezaji wao wapya na shamrashamra ambazo tumeziandaa naamini watu 60,000 bila mapengo watakuwa pale uwanja wa Taifa full muziki."

Pamoja na burudani nyingine, Simba inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Power Dynamo ya Zambia

Mchezo huo utapigwa saa 11 na nusu jioni baada ya utambulisho wa kikosi cha Simba

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’