Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa sapoti waliyompa wakati wote aliokuwa Msimbazi
Okwi aliyesajiliwa na Ittihad Sc ya Misri amesema anajisikia fahari kupata nafasi ya kuitumikia Simba na kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa na mashabiki wa timu hiyo
"Nawashukuru kwa kumbukumbu nzuri tuliyojenga kwa miaka mingi pamoja. Mlinichukulia mimi kama mwenzenu, niwahakikishie natambua mapenzi yenu nliyonionyesha," ameandika Okwi kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
"Nwashukuru viongozi na benchi la ufundi pia ambao walifanya kazi kubwa kuhakikisha tunapata mafanikio tuliyoyapata"
"Ingawa nimejiunga na Ittihad Sc, Simba itaendelea kubaki moyoni mwangu"
Okwi ameitumikia Simba kwa nyakati tatu tofauti katika kipindi cha miaka 10