Usajili wa Kwasi bado pasua kichwa, Lipuli yamuonya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
19 Dec 2017
Usajili wa Kwasi bado pasua kichwa, Lipuli yamuonya
Sakata la mchezaji Asante Kwasi anayetajwa kusajiliwa na klabu ya Simba lakini hadi sasa klabu ya Lipuli haijui mchezaji huyo yupo wapi.

Uongozi wa Lipuli umesema unasubiri maelezo kutoka kwa Kwasi juu ya kuchelewa kujiunga na kambi baada ya ruhusa aliyopewa kumalizika lakini bado hajarejea na hakuna taarifa yoyote aliyotoa kwa uongozi wake.

Mwenyekiti wa Lipuli Ramadhani Mahano ametoa sababu kadhaa akieleza kwa nini Lipuli inasema Kwasi ni mchezaji wao halali.

“Tuliingia mkataba na Kwasi Julay 30, 2017 tuna mkataba wa mwaka mmoja, mkataba wake unaisha Julai 29, 2018.

"Kwa maana hiyo inaonesha kwamba Simba watakuwa wamekiuka vipengele vingi vya usajili, ieleweke kwamba mchezaji yoyote ambaye bado anamkataba wa zaidi ya miezi sita na klabu yake kanuni za TFF na FIFA haziruhusu mchezaji huyo kuongea na klabu yoyote juu ya usajili.”

“Singida waliandika barua lakini walitoa ofa ya shilingi 10 miloni kwa sababu ofa yao ilikuwa chini sana tulishindwa hata kuwajibu kwa hiyo tukawa tunawasikiliza kama wataongeza ofa yao ili tuweze kufanya mazungumzo. Sisi tulihitaji juu ya hapo ili aweze kuondoka na kwenda kuitumikia klabu yoyote.”

“Bado hatujakutana kamati ya utendaji kwa sababu tunapenda kukaa pamoja, kwa hiyo tutasikiliza kama kuna klabu itakuja au kuonesha nia ya kumchukua tutakaa chini na kupanga tutamtoa Kwasi kwa kiasi gani cha pesa.”

“Baada ya kusikia tetesi zote hizo, mnamo December 12, 2017 klabu ya Lipuli tuliandika barua TFF tukitoa angalizo kwa vilabu vyote ambavyo vinajaribu kurubuni wachezaji wetu akiwemo Asante Kwasi juu ya kusajiliwa na klabu yoyote.”

“Hakuna klabu yoyote iliyokuja hadi sasa kwa ajili ya mazungumzo ya kumsajili Kwasi kwa hiyo, sisi klabu ya Lipuli hatuna la ziada isipokuwa tunasubiri TFF ibandike majina ya wachezaji wote waliosajiliwa baada ya dirisha dogo kufungwa na watangaze muda wa pingamizi ambapo sisi tutapinga usajili wowote ambao utakuwa umefanywa ukimuhusisha mchezaji huyo.

"Barua tuliyoiandikia TFF itakuwa ushahidi na tutakuwa tayari kwenda kuonesha vielelezo vyetu vinavyotufanya tuseme Kwasi ni mchezaji wetu halali.”

Inaelezwa kwamba, baada ya mchezo wa Simba dhidi ya Lipuli Kwasi alipewa ruhusa ya wiki mbili kwenda nyumbani kwao Ghana kuhudhuria mazishi ya baba yake.

Alitarajia kuwasili Iringa December 16, 2017.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE →