Kesho August 04 timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itashuka dimba la Kasarani nchini Kenya kuchuana na wenyeji wao Harambee Stars katika mchezo wa marudiano wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za CHAN 2020 kwa wachezaji wa ndani
Uongozi wa Simba utawarejesha nchini haraka wachezaji wake walio timu ya Taifa baada ya mchezo huo
Ikumbukwe August 06 Simba itachuana na Power Dynamo kwenye mchezo Tamasha la Simba Day kabla ya kusafiri kwenda nchini Msumbiji kuikabili UD Songo August 10
Kutokana na ufinyu wa muda, kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Patrick Aussems amewataka nyota wake watano warejee haraka baada ya mchezo
Wachezaji wa Simba waliosafiri nchini Kenya na timu ya Taifa ni Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassan Dilunga na nahodha John Bocco
Mlinda lango Aishi Manula na Ibrahim Ajib wameachwa jijini Dar es salaam baada ya kuumia