Imeelezwa usiku wa Disemba 15 ambayo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa vilabu kukamilisha usajili wa dirisha dogo lililofunguliwa Novemba 15, kulitokea hitilafu kwenye mtandao wa usajili wa FIFA (TMS) na hivyo kupelekea vilabu kushindwa kukamilisha zoezi hilo.
Sasa TFF imeviagiza vilabu kuhakikisha vinakamilisha zoezi la usajili ifikapo Disemba 23.
Aidha kwa kuwa mfumo huo wa TMS bado haujatengemaa, TFF imeziagiza klabu kuwasilisha nyaraka za usajili wa dirisha dogo moja kwa moja katika ofisi za Makao Makuu ya shirikisho hilo, Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema TFF inaendelea na jitihada za kuwasiliana na Mwendeshaji wa mfumo huo waliokasimiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) walioko Tunis, Tunisia ili kutatua tatizo hilo la kimtandao haraka iwezekanavyo ili kuweza kukamilisha usajili wa dirisha dogo.

ADVERTISE HERE