Klabu ya Simba imepata pigo kubwa leo Jumatatu, baada ya kuondokewa na mwanachama wao maarufu anayejulikana kwa jina la Fii Kambi kutokana na ugonjwa wa malaria.
Makamu wa Rais wa Simba, Iddy Kajuna amethibisha taarifa za kifo hicho na kusema, wamepoteza mtu muhimu aliyekuwa na mchango mkubwa ndani ya klabu.
"Aliipenda sana Simba, alijitolea kwa hali na mali popote ambapo ilikuwa inaenda kucheza, alitamani iwe na mafanikio, aliumia pindi ilipokuwa inafungwa,hakika tutamkumbuka kwa uhamasishaji wake,"anasema Kajuna na kuongeza.
"Msiba upo mtaa wa Jaribu Magomeni, jijini Dar es Salaam, taratibu nyingine zinaendelea kupangwa hivyo tutazidi kuwajulisha namna itakavyokuwa."
Mungu ailaze raho yake mahali pema peponi, AMEN

ADVERTISE HERE