Manara ataka utulivu Simba

Shabiki Waukweli By Shabiki Waukweli
β€’
25 Sep 2017
Manara ataka utulivu Simba
Mkuu wa Kitengo cha Habari Simba, Haji Manara anewataka mashabiki wasiingilie majukumu ya kocha, wampe nafasi kwa kocha afanye kazi yake kwa weledi.

Kufuatia matokeo ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mbao FC, baadhi ya mashabiki wamekuwa wakishinikiza uongozi wa Simba ufanye mabadiliko kwenye benchi la ufundi.

Hata hivyo Manara amesisitiza ni vizuri kocha akaachwa huru kufanya kazi yake kwa kuwa yeye ndiye mwenye taarifa sahihi juu ya kila mchezaji na utayari wake wa kuitumikia Simba katika mechi husika.

"Unajua mashabiki wanapaswa kujifunza na ikiwezekana kuwa watulivu na kuiacha taalum ifanye kazi. Mfano suala la sub linaweza kuwa limewaudhi, lakini hawajawahi kwenda mazoezini," amesema.

"Walimu ndiyo wanajua nani anafanya vizuri, nani wakimtumia kwa wakati gani itakuwa sahihi na si mashabiki wanamshabikia nani"

"Lakini hiyo haitoshi, kila mmoja anakumbuka, sisi ndiyo tulikuwa tunaongoza kuwafukuza makocha na ikawa si kitu kizuri. Sasa hatuwezi kuwa kitu kidogo, kocha aondoke.

"Tunaweza kupata kocha mzuri kabisa na maarufu, lakini pia asipate matokeo tunayotaka. Hii nayo itaturudisha nyuma na kuongeza maneno tena, hivyo ni lazima kutafakari mambo na ikiwezekana kuangalia utatuzi sahihi wa tatizo. Kufukuza au kuajili si njia pekee ya kumaliza tatizo, ameongeza Manara

Simba iko mkoani Shinyanga ambapo Jumapili ijayo itakuwa ugenini kumenyana na Stand United.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’