Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kimeondoka nchini Afrika Kusini leo baada ya kumaliza kambi ya wiki mbili iliyokuwa maalum kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Simba imebainisha kuwa timu itawasili nchini saa 12:20 jioni
"Kikosi cha Mabingwa wa nchi kinaanza safari muda huu kurejea nyumbani Tanzania kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kutoa burudani ya ukweli, burudani ya kibingwa katika Simba Day 6/8/2019 Uwanja wa Taifa"
"Kikosi kitatua Dar kwa ndege saa 12:20 jioni kikitokea Johannesburg, Afrika Kusini"


ADVERTISE HERE