Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ameupongeza uongozi wa klabu hiyo kwa kuwapatia mazingira mazuri ya kujiandaa na msimu mpya nchini Afrika Kusini
Akizungumza baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Orlando Pirates ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, Aussems alisema kambi waliyoweka Rustenburg ilikuwa bora kwani imewasaidia kufikia malengo waliyojiwekea
"Tulikuwa na kambi bora Rustenburg, tulipata kila tulichokihitaji, hakika tulikuwa na wiki mbili nzuri sana za maandalizi," amesema
Aidha Aussems amewapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri mchezo dhidi ya Orlando Pirates
"Tumemaliza kambi na Orlando Pirates ambao wapo tayari kuliko sisi lakini tumecheza vizuri"
"Napenda kuwapongeza wachezaji wangu tulikuwa na wakati mzuri sana Rustenburg, kila mmoja kafanya kazi nzuri tunaweza kusema hii kambi imekuwa nzuri sana na nimeridhishwa"
Simba inarejea nchini kesho kujiandaa na Tamasha la Simba Day na baadae kuelekea Msumbiji kuikabili UD Songo kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya awali utakaopigwa August 10