SportPesa Simba Week yazinduliwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Jul 2019
SportPesa Simba Week yazinduliwa

Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Crescentius Magori leo ametangaza kuwa wiki ya Simba itaanza rasmi keshokutwa Jumatano, Julai 31 na itahitimishwa uwanja wa Taifa August 06 kwa mchezo wa kukata na shoka kati ya Simba dhidi ya Power Dynamo

Maadhimisho ya mwaka huu ambayo inatimia miaka 10 yamedhaminiwa na kampuni ya SportPesa na yatafahamika kama SportPesa Simba Week

Aidha Magori pia amesema kikosi cha Simba kitarejea nchini keshokutwa baada ya kumaliza maandalizi yake huko Afrika Kusini

Simba pia inatarajiwa kusaini mkataba na udhamini wa jezi na vifaa vya michezo ambapo uongozi wa timu hiyo utabainisha faida zitakazopatikana kutokana na mkataba huo

"Wiki ya Simba itaanza 31/7/2019 wachezaji watarejea kutoka Nchin Afrika kusini Siku hiyo hiyo tutasaini mkataba na mdhamini wa jezi mkataba ni wa miaka miwili, muda utakuwa saa tano asubuhi hapahapa Serena

Tutaweka wazi kila kitu pia Siku hiyo hiyo saa sita usiku Simba itatangaza jezi mpyaa ya msimu ujao zipo 3 ambazo zitaanza kuuzwa tarehe
1 August

Wakati tuna saini tutawajuza maduka gani yatauza jezi nchi nzima. Tarehe hiyo tutazungumza na wanahabari hapa hapa tutazindua Kadi mpyaa za klabu ambazo ni za kielektroni

Tutaeleza kila kitu kuhusu hizo kadi, Fans card ndio hii card baadae zitamuwezesha mwanachama kujiunga. Siku hiyo hiyo tutaanza kuuza card za vingilio. tutakuwa na platinum za aina mbili ambazo ni 150,000/= pamoja na 100,000/="

Kuhusu maandhimisho ya wiki ya Simba;

"Tarehe 2 August 2019 Sport Pesa watatembelea watoto yatima, huku Simba ikitembelea Hospitali ya Ocean road

Tunawaomba wana Simba tarehe tatu nchi nzima wafanye tendo hili la kuchagua hospitali na kuwajulia hali wagonjwa saa tatu asubuhi

Tunampango wa kuchangia damu na tutawajulisha vituo vikubwa. Wenzetu wafanye hivyoo hospitali kubwa, pia tarehe 3 hiyo tutazindua wimbo wa klabu ambao hadi hivi sasa unaandaliwa"

Siku ya Simba Day

"Siku hiyo tutaanza burudani mapema sana. Tutakuwa na wasanii wengi sana wakiongozwa na Twanga pepeta

Mechi zitakuwa tatu. Simba Queens wataanza wakifuatiwa na under 20 njoo uone wakicheza na fountain academy. Patafuatiwa na utambulisho wa wachezaji Haji Manara atahusika katika utambulisho huo.

Siku hiyo hiyo Simba Queens watatembelea sekondari ya Makongo kuhamasisha wasichana pale

Tarehe sita sasa watu wote wavalie jezi nyekundu. Tunafanya utaratibu wenzetu wa viwanja vikubwa huko mikoani waweze kuweka screen kubwa wakusanyike na kuona"

Kauli ya SportPesa, imetolewa na Tarimba

"Kikubwa tunawapongeza simba. Wamekuwa na mwendelezo mzuri sana wa Simba week na Sportspesa wameona wiki hii iitwa Sportspesa Simba Wiki.

Naona fahari sana kujihusisha vizuri japo nikitoka hapa mnajua wenyewe. Simba imetutoa kimasomaso ukanda wetu na Sportspesa inaona fahari sana.

Nasisi Sportspesa ni rasmi sasa simba inauza jezi zake si kwa kutundika kwenye miti.

Sitoi dongo upande mwingine. Tunatoa wito kuhakikisha wananunua jezi mapema ili kuondoa mkanganyiko, nunueni kwa wingi jezi na tutapromote kwa kasi sana"

Kauli mbiu itakayotumika Simba Week ya mwaka huu ni IGA UFE THIS IS NEXT LEVEL

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
2h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
3h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
5h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’