Manula vs Kakolanya patachimbika

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Jul 2019
Manula vs Kakolanya patachimbika

Mlinda lango Beno Kakolanya ameendelea kufanya vitu adimu Afrika Kusini na kumpa mtihani mkufunzi wa Simba Patrick Aussems kuamua nani atakuwa chaguo la kwanza kati yake na Aishi Manula

Mpaka sasa kakolanya ameonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mazoezi

Juzi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Township Rollers alionyesha makali yake kwa kudaka mkwaju penati huku akiokoa mashambulizi kadhaa

Hata hivyo hatakuwa na kazi rahisi kupata nafasi mbele ya Aishi Manula ambaye kwa miaka miwili sasa amejipambanua kuwa kipa namba moja wa Simba na timu ya Taifa

Manula amelinda ubora wake kwa muda wote huo

Kakolanya amesema yeye atatimiza wajibu wake akipewa nafasi, jukumu la kuamua nani acheze litabaki kwa kocha mwenyewe

cut

"Suala la namba kwa sasa sio kipaumbele changu kwa kuwa mimi sipangi kikosi hilo lipo mikononi mwa mwalimu cha msingi ni mashabiki kuzidi kutuombea," amesema

Ushindani baina ya makipa hao utainufaisha zaidi Simba kwani ni dhahiri utaboresha viwango vyao

Lakini ushindani wa namba hautakuwa kwa magolikipa tu, usajili uliofanywa na Simba uliangalia zaidi kuwa na kikosi kipana ambacho kitakuwa na wachezaji wote wenye uwezo

Karibu kila nafasi Simba ina wachezaji wawili ambao wanaweza kuanza kikosi cha kwanza

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’