Mfadhili wa zamani wa klabu ya Simba Azim Dewji amelazwa Hospitali ya Muhimbili Taasisi ya Mifupa (MOI) baada ya kuumia ajalini akiwa njiani kwenda Rufiji katika uwekaji jiwe la msingi mradi wa umeme wa Rufiji, juzi
Inaelezwa hali yake inaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu akiwa amepata madhara katika uti wake wa mgongo
Dewji ana historia kubwa katika klabu ya Simba
Mwaka 1993 akiwa mfadhili wa Simba, aliwawezesha mabingwa hao wa Tanzania Bara kufika fainali ya michuano ya kombe la Washindi (sasa Shirikisho) wakipoteza kwa kufungwa na Stella Abidjan
Ni mmoja wa wadau waliotoa mchango mkubwa katika mabadiliko yaliyofanywa na klabu ya Simba kutoka mfumo wa uendeshaji wa zamani kwenda kampuni
ADVERTISE HERE