Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo wanashuka dimbani huko Afrika Kusini kucheza mchezo wa tatu wa kirafiki dhidi ya Township Rollers, mabingwa wa ligi kuu ya Botswana
Kulingana na taarifa iliyotolewa na uongozi wa Simba jana, mchezo huo utapigwa kuanzia saa nne asubuhi muda wa Afrika Kusini, kwa Tanzania itakuwa ni saa tano
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema michezo ya kirafiki inamsaidia kubaini mapungufu ya kikosi chake na kuyarekebisha kabla ya kuanza msimu mpya
"Sijali sana matokeo, ninachoangalia ni kwa kiasi gani wachezaji wangu wameelewa kile ninachowafundisha mazoezini," amesema
Simba tayari imecheza michezo miwili Afrika Kusini na kufanikiwa kushinda yote kwa kufunga mabao manne kwenye kila mchezo
ADVERTISE HERE