Beki wa kulia wa Simba Shomari Kapombe amesema baada ya kupona majeraha ya goti yaliyomuweka nje kwa muda mrefu, ameanza kurejeshwa kikosini kwa utaratibu maalum
Kapombe ambaye tayari ameanza kufanya mazoezi na wachezaji wengine, amesema kocha ameanza kumpa nafasi ya kucheza taratibu
"Kwanza kikubwa namshukuru Mwenye ez Mungu kwamba mpaka sasa hali yangu naendelea vizuri, naendelea na mazoezi vizuri na nafanya mazoezi na timu" amesema
"Kikubwa kwanza kocha alianza kunichezesha dakika 30, nikacheza dakika 60 kwa hiyo ninakoelekea nitaweza kucheza dakika 90"
"Naenda hatua kwa hatua lakini nina imani muda utakuja nitacheza dakika 90, naamini Mungu atanisaidia kuweza kuwa fiti"
"Maandalizi tunayofanya ni mazuri na yanamuandaa kila mchezaji kuwa katika hali nzuri kwa ajili msimu unaokuja pamoja na Tamasha la Simba"