Wakati mashabiki wa Simba wakiwa bado na huzuni ya kumpoteza kiungo James Kotei aliyetimkia Kaizer Chiefs, benchi la ufundi la timu hiyo limewatoa hofu kwa kuwa nafasi yake imepata mtu sahihi
Nae si mwingine, ni Sharaff Elden Shiboub aliyesajiliwa kutoka klabu ya El Hilal ya Sudan
Shiboub ameonyesha uwezo mkubwa kwenye mazoezi ya Simba yanayoendelea Afrika Kusini
Adel Zrane, ni kocha wa viungo wa klabu ya Simba, anaamini uwezo wa Msudani huyo utaisaidia Simba kwenye michuano mbalimbali msimu ujao
Licha ya kumnoa kwa muda mfupi, Zrane amekubali Shiboub ni jembe hasa
"Nimemuangalia Eldin kwa muda mchache tuliokaa huku Afrika Kusini , nimegundua ana uwezo mkubwa sana," amesema
"Ni mzuri sana kwenye kukaba na ana nidhamu ya hali ya juu katika maamuzi yake"
"Nimefurahishwa sana na uwezo wake, endapo atakuwa fiti kwa msimu mzima basi atakuwa msaada mkubwa kwetu"
cutShiboub alitua Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea klabu ya El Hillal ya nchini Sudan
Usajili wake ni pendekezo la kocha Patrick Aussems ambaye alimfahamu kupitia Mawakala huko Sudani
Ni mchezaji mwenye uzoefu wa soka la Afrika kuanzia ngazi ya vilabu mpaka timu ya Taifa
Shiboub (24) ameitumikia timu ya Taifa ya Sudan tangu akiwa na umri wa miaka 17