Licha ya kupoteza mchezo wa fainali ya kombe la Chalenji, kocha mkuu wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Ali ‘Morocco amesema, anajivunia mafanikio aliyoyapata ikiwa ni kuifikisha fainali timu yake ingawa hakufanikiwa kutwa taji hilo.
“Mimi ni kocha mdogo kuliko makocha wote, nimeweza kuifikisha timu fainali najivunia sana kwa mafanikio tuliyopata ukilinganisha na timu nyingine zilivyojiandaa na timu yetu ilivyokuwa underdogs imeweza kufika fainali si kitu cha kubeza.â€
Morocco amewashukuru watanzania wote kwa ujumla kutokana na kuiunga mkono Zanzibar tangu hatua ya makundi hadi fainali.
“Tunawashukuru watanzania wote kwa kipindi chote ambacho tulikuwa kwenye mashindano haya kwa kutupa support na kututia moyo, nafikiri tumeweza kuonesha kwamba tunaweza kupambana kwa hiyo maisha yanaendelea baada ya fainali hii tutajipanga ili kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi katika mashindano mengine.â€
Bingwa wa mashindano hayo (Kenya) wamezawadiwa kombe, medali pamoja na dola za Marekani 30,000 wakati washindi wa pili (Zanzibar Heroes) wakipatiwa medali na dola 20,000 huku washindi wa tatu (Uganda) wakipewa medali na dola 10,000.

ADVERTISE HERE