Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars Ndayiragije Etienne amemteua Mshambuliaji wa Simba John Bocco kuwa nahodha wa timu ya Taifa kwa wachezaji wa Ndani
Aidha, kulingana na taarifa iliyotolewa na TFF, Bocco atasaidiwa na wakongwe Juma Kaseja, Kelvin Yondani na Erasto Nyoni
Stars inajiandaa na mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi ya michuano ya CHAN dhidi ya Kenya utakaopigwa Jumapili, Julai 28 kwenye uwanja wa Taifa
Bocco na wachezaji wengine sita wa Simba walitua kambi ya Stars juzi wakitokea kwenye kambi ya Simba Afrika Kusini
ADVERTISE HERE