Beki mpya wa Simba Gerson Fraga Vieira anaelekea kumshawishi kocha Patrick Aussems ambaye ameonyesha kuvutiwa na aina yake ya uchezaji
Fraga raia wa Brazil aliyetua Simba akitokea nchini India, amekuwa chaguo la kwanza kwenye safu ya ulinzi akianza sambamba na Paschal Wawa kwenye michezo ya kirafiki
Aidha hata katika mazoezi, mara nyingi Aussems anawapanga Fraga na Wawa pamoja
Simba imeongeza wachezaji wanne kwenye safu yake ya ulinzi ambao ni Gadiel Michael, Fraga, Kennedy Juma na Tairone Santos aliyesajiliwa kutoka Brazil
Walinzi hao wameungana na Mohammed Hussein, Yusufu Mlipili, Paschal Wawa na Erasto Nyoni ambao wameendelea kubaki Msimbazi baada ya kuongeza mikataba
Safu ya ulinzi ni eneo ambalo Aussems ameweka mkazo zaidi msimu huu
Simba imedhamiria kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa hivyo ni lazima kuwa na safu imara ya ulinzi
Licha ya mafanikio ya kutinga hatua ya robo fainali msimu uliopita, safu ya ulinzi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara haikuwa imara sana kwani waliruhusu mabao mengi kwenye michezo yote ya ugenini