Beki wa kati wa Simba, Paschal Wawa, amesema wachezaji wapya waliosajiliwa katika kikosi hicho kuelekea msimu ujao, ni muziki mnene.
Wekundu wa Msimbazi hao wanakabiliwa na michuano ya Ligi Kuu Tanzania na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba ni Wabrazil Tairone Santos da Silva, Gerson Fraga Viera na Wilker Henrique da Silva.
Wengine ni Francis Kahata (Mkenya), Deo Kanda (DR Congo) na Sharaf Shiboub (Msudan), huku wazawa wakiwa ni Ibrahim Ajib, Gadiel Michael, Beno Kakolanya, Miraji Athuman na Kenedy Juma.
Wawa amesema wachezaji wapya wanaonyesha kiwango cha hali ya juu katika mazoezi yao yanayoendelea nchini Afrika Kusini
Wawa alisema kila mchezaji, anaonekana anajua kucheza soka, hivyo anaamini msimu ujao utakuwa mzuri kwao kuhakikisha wanatetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Bara na kufika mbali kimataifa.
"Kikosi chetu kipo vizuri, nyie wenyewe mtawaelewa vizuri uwanjani msimu ukianza," Wawa amenukuliwa na gazeti la Bingwa