Simba kujipima na wababe wa Yanga kesho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Jul 2019
Simba kujipima na wababe wa Yanga kesho

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba bado wako Afrika Kusini wakiendelea na maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara, ligi ya mabingwa pamoja na michuano mingine

Wakiwa huko Afrika Kusini, Simba tayari wamecheza michezo miwili ya kirafiki na kufanikiwa kushinda yote huku wakifunga mabao nane

Mchezo wa kwanza ulikuwa dhidi ya Orbit Tvet, Simba ikishinda mabao 4-0 kabla ya juzi kuifumua Platinum Stars mabao 4-1

Kesho mabingwa hao wa nchi, watachuana na mabingwa wenzao kutoka Botswana Township Rollers

Hawa Rollers ndio waliwaondoa Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa mapema mwaka jana kwa kuwachapa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Watakuja tena Tanzania mwaka huu kumenyana na Yanga katika hatua ya awali

Nao wameweka kambi yao ya maandalizi Afrika Kusini

Simba itakamilisha ratiba yake ya michezo ya kirafiki Julai 30 kwa kuumana na Orlando Pirates ambao msimu uliopita walimaliza katika nafasi ya pili ligi kuu ya Afrika Kusini

Pirates itashiriki michuano ya ligi ya mabingwa kama ilivyo kwa Simba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’