Wachezaji saba wa Simba walioitwa kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa, wameingia kambini leo baada ya kuwasili kutoka Afrika Kusini
Nahodha John Bocco, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Gadiel Michael, Hassan Dilunga na Ibrahim Ajib wote wameingia kambini tayari kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo dhidi ya Kenya Julai 28
Akizungumza baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, mkongwe Erasto Nyoni amesema wamerudi nchini kuongeza nguvu katika kikosi cha Stars ili kuhakikisha wanalipa kisasi kwa Kenya
Nyota hao wamewaacha wenzao wakiendelea kujifua Afrika Kusini
ADVERTISE HERE