Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema msimu ujao anataka timu yake iwe na uwezo wa kucheza mfumo zaidi ya mmoja
Katika michezo miwili ya kirafiki, Aussems aliwabadilisha majukumu baadhi ya wachezaji huo ukiwa ni mpango wa majaribio yake
Akizungumza leo baada ya Simba kuichapa Platinum Stars mabao 4-1 kwenye mchezo wa kirafiki, Aussems amesema anataka wachezaji wake wawe na uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja
"Kwa sasa nataka kuona wachezaji wakicheza nafasi zaidi ya moja sababu huu msimu nataka kuwa na mifumo miwili au mitatu," amesema
Baada ya ushindi kwenye michezo miwili ya kirafiki iliyopigwa jana na leo, kesho kikosi cha Simba kinaendelea kujifua huko Afrika Kusini
Mchezo wa kirafiki unaofuata, utapigwa Julai 27 dhidi ya Township Rollers