Bwalya aiponyoka Simba, atua Misri

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Jul 2019
Bwalya aiponyoka Simba, atua Misri

Walter Bwalya Mshambuliaji wa Nkana Fc aliyekuwa akiwaniwa na Simba, mabingwa wa soka Tanzania Bara, amejiunga na timu ya Gouna Fc inayoshiriki ligi kuu ya Misri

Kulingana na taarifa iliyoripotiwa na vyombo vya habari nchini Zambia leo, El Gouna imelipa kitita cha Dola 650,000 ambazo ni zaidi ya Bilioni 1.5 kuinasa sahihi ya mshambuliaji huyo aliyeibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya Zambia mwaka 2016

Wakala wa mchezaji huyo Patrick Chikoye amethibitisha kuwa mteja wake alikuwa na ofa kadhaa lakini wameafikiana na El Gouna inayomilikiwa na familia ya Sawiris ambao ni matajiri wa kutupwa

Familia hiyo inamiliki timu ya ligi daraja la kwanza huko Uswisi (Fc Luzern) pia hivi karibuni wameinunua klabu ya Aston Villa iliyopanda ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita

Walter yuko nchini Misri kwa zaidi ya wiki moja ambapo inaelezwa alianza kujifua na timu hiyo jana

Baada ya kumpoteza Bwalya, matumaini ya kumsajili Justine Shonga wa Orlando Pirates nayo yamekuwa madogo Simba ikihitaji kutoa dau kubwa zaidi ya Zamalek inayodaiwa kuweka mezani dau la dola milioni moja (Zaidi ya Bilioni 2 za Kitanzania)Β  ili kumsajili mshambuliaji huyo

Hata hivyo inaelezwa Shonga hajaridhia kujiunga na mafarao hao lakini kikwazo kinabaki kwenye mkataba wake na Orlando Pirates

Pirates wameonyesha wako tayari kumuuza kwa timu itakayofika dau

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’