Aussems atumia vikosi viwili mechi dhidi ya Orbret Tvet

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Jul 2019
Aussems atumia vikosi viwili mechi dhidi ya Orbret Tvet

Simba leo imecheza mchezo wake wa kwanza Afrika Kusini na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Obret Tvet

Mchezo huo uliopigwa uwanja wa hoteli ya The Rayol Marang, nahodha John Bocco alipachika mabao mawili huku Hassan Dilunga na mshambuliaji raia wa Brazil Wilker Da Silva wakifunga mengine mawili

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems alitumia mchezo huo kusaka wachezaji wa kuingia kwenye kikosi chake cha kwanza

Simba itacheza michezo mingine mitatu ambayo bila shaka itamsaidia Aussems kupata kikosi cha kwanza

Kesho Simba itashuka tena dimbani kupambana na Platinum Stars inayoshiriki ligi daraja la kwanza hukohuko Afrika Kusini

Katika mchezo wa leo Aussems alitumia vikosi viwili tofauti

Kikosi kilichoanza kilicheza kwa dakika 60 na kiliwajumuisha Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Fraga, Nyoni, Mzamiru, Mkude, Miraji, Dilunga, Bocco na Ajib

Kipimo kikubwa cha kwanza kwa Simba ni mchezo wa Jumamosi Julai 27 dhidi ya mabingwa wa Botswana, Township Rollers na kisha kumaliza na Orlando Pirates Julai 30

Simba inatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam mwanzoni mwa mwezi wa nane tayari kwa Tamasha la SIMBA DAY ambalo limepangwa kufanyika August 06

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
34m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’