Uongozi wa Simba umerudisha nyuma Tamasha la SIMBA DAY ambapo sasa litafanyika August 06 kwenye uwanja wa Taifa
Kama ilivyo kawaida yake, siku hiyo Simba itatambulisha kikosi kwa kucheza mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Power Dynamos na Zambia
Aidha maadhimisho ya wiki ya Simba yataanza August 01 na kufikia Tamati August 06
Uamuzi huo umechukuliwa ili kuwapa nafasi mabingwa hao wa Tanzania Bara kuwahi kusafiri kwenda Msumbiji kwa ajili ya mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya UD do Songo
Mchezo huo utapigwa kati ya August 09, 10 au 11

ADVERTISE HERE