Wachezaji saba wa Simba ambao walikuwa Afrika Kusini kwenye kambi ya klabu hiyo, wanatarajiwa kuripoti kambi ya Stars leo
Stars iliingia kambini juzi kwa ajili ya maandalizi ya michezo miwili dhidi ya Kenya, Julai 28 na August 04
Nyota hao wakiongozwa na nahodha John Bocco wanaondoka Afrika Kusini leo kuitikia wito wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF)
Wengine ni Aishi Manula, Gadiel Michael, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Hassani Dilunga na Ibrahim Ajib
ADVERTISE HERE