Baada ya kufanya mazoezi kwa takribani wiki moja huko Afrika Kusini, kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo kitashuka dimbani kucheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Orbit Tvet
Timu hiyo inamilikiwa na Chuo Kikuu cha Orbit na unatarajiwa kupigwa saa tano asubuhi
Huo ni moja ya michezo minne ambayo Simba itacheza Afrika Kusini
Kesho Jumatano itacheza na Platinum Stars na siku ya Jumamosi itaumana na Township Rollers, wababe wa Yanga
Simba itamaliza ratiba yake Julai 30 kwa kuumana na vigogo wa soka Afrika Kusini Orlando Pirates
ADVERTISE HERE