Wachezaji saba walioitwa Stars wamuumiza kichwa Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Jul 2019
Wachezaji saba walioitwa Stars wamuumiza kichwa Aussems

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems anakabiliwa na changamoto ya kukiandaa kikosi chake bila ya wachezaji saba walioitwa kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'

Stars iliingia kambini jana kuanza maandalizi ya mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za michuano ya CHAN dhidi ya Kenya

Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa Julai 28 na kisha timu hizo kurudiana August 04 nchini Kenya

Akizungumza baada ya CAF kutoa ratiba ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa, Aussems amesema anakabiliwa na changamoto hiyo kutokana na umuhimu wa wachezaji hao kuelekea mchezo wa kwanza dhidi ya UD Songo ambao utapigwa mapema tofauti na matarajio yao

"Ni pigo kwetu kwa sababu hatutakuwa na wachezaji saba mpaka August 07 siku mbili kabla ya kucheza na UD Songo," amesema

"Tunalazimika kufanya mabadiliko ya maandalizi yetu ili kuhakikisha tunakuwa tayari kwa mchezo huo"

Wachezaji wa Simba walioondoka Afrika Kusini kurejea nchini kuungana na kambi ya Stars ni Aishi Manula, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassani Dilunga, Ibrahim Ajib na nahodha John Bocco

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
16h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
20h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’