Kitendo cha Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) kuipanga Simba hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa, kimevuruga ratiba ya timu hiyo kuelekea Tamasha la SIMBA DAY linalofanyika kila mwaka
Simba inapaswa kusafiri kwenda nchini Msumbiji kuumana na UD Songo katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ambao utapigwa kati ya tarehe 09, 10 au 11 mwezi wa nane
Hivyo hakuna uwezekano SIMBA DAY kufanyika August 08 kama lilivyofanyika miaka yote
Hata hivyo msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema Tamasha hilo litafanyika, lakini huenda kutakuwa na mabadiliko ya tarehe
ADVERTISE HERE