Nyota Simba wajiongezea dozi ya mazoezi Afrika Kusini

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Jul 2019
Nyota Simba wajiongezea dozi ya mazoezi Afrika Kusini

Nahodha wa Simba, John Bocco Adebayor’, Mnyarwanda Meddie Kagere na Mkenya Francis Kahata ni kama wameshtukia jambo katika kambi ya timu yao iliopo nchini Afrika Kusini na kuamua kuliamsha mapema ili wanoge zaidi.

Nyota hao ambao wote ni washambuliaji wameamua kufanya mazoezi yao binafsi ya kufa mtu kabla ya kuungana na wenzao kwenye gym iliyopo ndani ya kambi yao vizuri inayojiandaa kuingia wiki ya pili tangu ilipoanza Jumatatu iliyopita.

Kagere aliyekuwa Mfungaji Bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara akifunga mabao 23 na Bocco aliyekuwa mfungaji wa pili ndani ya Simba nyuma ya Kagere kwa mabao yake 16 sambamba na Kahata ingizo jipya Msimbazi, wamekuwa wakifua wenyewe kama njia ya kujiweka fiti zaidi.

Nahodha Bocco huingia kwenye mazoezi hayo mapema saa 9:00 alasiri saa za Tanzania, kisha akafuata Kagere akafuata saa 9:15 na baadaye Kahata naye akatimba saa 9:20.

Walipododoswa, sababu ya kufanya hivyo Bocco alisema;

"Naenda kwanza gym kujiweka sawa baada ya hapo ndio nitaungana na wenzangu"

Nae Kagere alisema;

"Napenda kuanza mazoezi binafsi kwa ajili ya kujiweka fiti, ninapokwenda kuungana na wenzangu nakuwa katika hali nzuri"

Simba huwa inaanza mazoezi yake ya jioni saa kumi

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’