Baada ya msimu uliopita mshambuliaji Meddie Kagere kutua Simba akitokea klabu ya Gor Mahia, msimu huu Simba imemleta 'mpishi' wake mkuu wa mabao Francis Kahata
Kagere na Kahata wakati wakiwa Gor Mahia, wakishirikiana na Jacques Tuyisenge ambaye ametimkia Angola, walitengeneza utatu wa hatari ambao uliwapa mafanikio mabingwa hao wa Kenya
Kahata ametua Simba kuongeza ubunifu kwenye safu ya kiungo
Kiungo huyo wa Kimataifa wa Harambee Stars ni fundi kwelikweli katika kupiga pasi za mwisho
Kagere kinara wa mabao kwenye ligi kuu msimu uliopita, kazi yake itakuwa rahisi sana msimu ujao
Kwani amezunguukwa na mafundi hasa wa kutengeneza nafasi za mabao
Pamoja na Kahata, Ibrahim Ajib, Hassani Dilunga na Clatous Chama nao watakuwa na jukumu la kufanya kazi ya washambuliaji kuwa nyepesi
Safu ya ushambuliaji ya Simba itaongozwa na washambuliaji watatu wa kati Meddie Kagere, John Bocco na Wilker Da Silva
Wakati Deo Kanda na Miraji Athumani hawa watakuwa wakitokea pembeni