Wakati Simba ikijiandaa kucheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Orbit Tvert keshokutwa huko Afrika Kusini, kocha Mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems amesifu mazingira ya kambi yao
Simba imeweka kambi katika Hoteli ambayo ilitumiwa na timu ya Taifa ya Uingereza kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 katika jiji la Rustenburg
Utulivu pamoja na upatikanaji wa mahitaji yote kwa ajili ya mazoezi, ni vitu vilivyomfanya kocha Aussems aamini wakitoka hapo watakuwa wameiva kwelikweli
Mabingwa hao wa Tanzania Bara waliwasili huko Afrika Kusini Jumatatu iliyopita na mpaka sasa wamejifua kwa siku sita
Julai 23 watacheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya timu ya Chuo Kikuu cha Orbit Tvert
Siku moja baadae, Julai 24 wataumana na Platinum Stars inayoshiriki ligi daraja la kwanza hukohuko Afrika Kusini
Simba itacheza michezo mingine miwili dhidi ya Tonship Rollers, mabingwa wa Botswana Julai 27 na Orlando Pirates Julai 30 kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini