Kwa kikosi hiki, ubingwa utarudi Msimbazi - Ajib

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Jul 2019
Kwa kikosi hiki, ubingwa utarudi Msimbazi - Ajib

Kiungo aliyerejea nyumbani, Ibrahim Ajibu amekiangalia kikosi cha Simba kilichopo nchini Afrika Kusini na kisha akatikisa kichwa na kusema ‘kwa chama hili tunakosaje ubingwa'

Mkali huyo wa asisti amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili kwenye dirisha hili kubwa la usajili akitokea Yanga ambayo iko kambini Morogoro.

Simba kwa sasa ipo kambini Sauzi ambapo ilikwenda huko Jumatatu iliyopita na imekuwa ikifanya mazoezi kwenye Mji wa Rustenburg chini ya kocha Mbelgiji, Patrick Aussems.

Simba imefanya usajili kwa kuongeza nyota kadhaa wapya wakiwemo Gadiel Michael, Mkenya Francis Kahata, Deo Kanda (DR Congo), Wabrazili Tairone Santos da Silva, Gerson Fraga Vieira na Wilker Henrique da Silva.

Pia imemsaini Msudani, Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman, Beno Kakolanya, Kennedy Juma huku pia ikiwaongeza mikataba nyota wao wa msimu uliopita kama Meddie Kagere, Clatous Chota Chama, John Bocco, Shomary Kapombe, Pascal Wawa, Aishi Manula na wengineo.

Ajib anaamini kikosi chao ni kizuri na kinaundwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu hivyo msimu ujao watafanya vizuri na hakutakuwa na sababu ya kushindwa kutwaa makombe.

"Simba iko vizuri kwa aina ya kikosi hicho ambacho kipo, hata ukiangalia wachezaji wake walivyo, kwa hiyo nina imani itafanya vizuri," Ajib aliliambia gazeti la Championi

Ajibu ambaye alikuwa nahodha wa Yanga msimu uliopita, amekiri kuwa hana uhakika kama atapata namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo

"Sijajua kama nitapata namba kwenye timu, tuwe tu wavumilivu lakini pia watu wasubiri kuona nini ambacho nitakifanya katika klabu yangu hii"

GPL

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
43m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’