Uongozi wa Simba umesema bado haujakamilisha usajili wa mchezaji mmoja ambaye umeahidi atakuwa 'sapraizi' kwa mashabiki wa timu hiyo
Ukiachana na Walter Bwalya ambaye amezungumzwa sana kuwaniwa na mabingwa hao wa Tanzania Bara, taarifa za uhakika ni kuwa Simba ambayo iko Afrika Kusini inawania saini ya mshambuliaji wa Orlando Pirates Mzambia Justin Shonga
Mpaka siku ya kesho Jumapili hatma ya nyota huyo huenda ikawa imefahamika
Kwani awamu ya pili ya dirisha la usajili wa ligi ya Mabingwa pamoja na faini, itafungwa rasmi kesho Julai 21 ambapo baada ya hapo mchezaji atakayesajiliwa ataruhusiwa kutumika kuanzia hatua ya makundi
Simba bado ina nafasi ya mchezaji mmoja wa kigeni baada kuamua kumtema mlinzi wa kulia Zana Coulibaly
ADVERTISE HERE