Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kinaendelea na maandalizi ya msimu mpya nchini Afrika Kusini leo wakiwa wameingia siku ya tatu tangu watue nchini humo
Wakiwa Afrika Kusini wababe hao wa soka la Tanzania wanatarajiwa kucheza michezo mitatu ya kirafiki
Mchezo wa kwanza utapigwa Julai 23 ambao bado timu watakayocheza nayo haijawekwa wazi
Lakini Julai 27 watacheza na mabingwa wa ligi kuu ya Botswana Township Rollers
Rollers iliwahi kuja Tanzania kucheza na Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na kuondoka na ushindi wa mabao 2-1
Mchezo mwingine utapigwa Julai 30
ADVERTISE HERE