Meddie Kagere alitua mapema jana Afrika Kusini akichelewa kuungana na kambi ya kikosi cha Simba nchini humo kutokana na changamoto ya pasi ya kusafiria
Hata hivyo mshambuliaji huyo bora wa Simba msimu uliopita, jioni alishiriki mazoezi na wachezaji wengine na kuonyesha ushindani sawa na wachezaji waliofika mapema
Katika mazoezi ya jioni jana ambayo kocha Patrick Aussems aligawa vikosi viwili, Kagere aliendeleza utamaduni wake wa kuzifumania nyavu
Baada ya Emmanuel Okwi kuondoka, Kagere na nahodha John Bocco wanatarajiwa kuibeba safu ya ushambuliaji ya Simba wakishirikiana na washambuliaji wapya Wilker Henrique, Ibrahim Ajib, Miraji Athumani na Deo Kanda
ADVERTISE HERE