Aussems kusuka ukuta wa 'Berlin' Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Jul 2019
Aussems kusuka ukuta wa 'Berlin' Simba

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems anaendelea kukifua kikosi chake huko Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya

Mabingwa hao watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara wana kazi ya kulinda ubingwa wao kwa msimu wa tatu mfululizo pamoja na kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ambayo msimu uliopita walitolewa hatua ya robo fainali

Moja ya eneo ambalo Aussems amekuwa akiliangalia zaidi ni safu ya ulinzi wa kati ambayo msimu uliopita ilikuwa ikiundwa na Juuko Murushid, Pascal Wawa, Erasto Nyoni Paul Bukaba na wakati mwingine anasaidia James Kotei.

Baada ya baadhi ya wachezaji hao kuondoka akiwamo Kotei, kuna mabeki wapya wamesajiliwa ambao wataziba mapengo hayo kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mabeki wapya wa kati walisajiliwa na Wekundu wa Msimbazi hao, kumuongezea nguvu Wawa na Nyoni, ni Wabrazil Tairone Santos da Silva na Gerson Fraga Viera pamoja na Mtanzania Kenedy Juma kutoka Singida United.

Wachezaji wote hao kulingana na maumbo yao na rekodi katika timu walizotoka, hakuna shaka kuwa watamudu mshike mshike wa kikosi hicho kinachopewa nafasi kuwa ya kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita.

Katika kuhakikisha mambo yanakwenda kama inavyotakiwa, Aussems ameanza mikakati mapema ya kutengeneza muunganiko wa mabeki hao kumtafutia Wawa Pacha wake.

Mbrazil Viera ndiye anayepewa nafasi kubwa  ya kutengeneza kombinesheni  kati yake na Wawa kutokana na mwalimu mara nyingi kuwaweka karibu karibu.

Viera ana uwezo mkubwa wa kuzuia mashambulizi na kukaba, pia ana nguvu, hivyo endapo ataelewana na Wawa, wakisimamishwa pamoja  katika safu hiyo, itakuwa ni ngumu kwa mastraika wa timu pinzani kupenya kirahisi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kambi ya Simba, kombinesheni ya mabeki hao inatarajia kujaribiwa katika mchezo wa kirafiki Julai 23, watapokipiga na Orlando Pirates.

Simba wanatarajia kucheza mechi tatu za kirafiki wakiwa nchini humo, lengo likiwa ni kuandaa kikosi cha kwanza kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, utakaopigwa  Agosti 17, mwaka huu.

Aussems amekiri kuwa msimu ujao ana kazi kubwa  ya kutetea ubingwa wao kutokana na ligi hiyo kuoneka itakuwa ya ushindani zaidi ya misimu iliyopita.

Alisema nafasi pekee ya kutengeneza kikosi bora ni katika kambi waliyopo Afrika Kusini kwa sababu baada ya hapo ratiba itakuwa imebana ya michuano ya ndani na kimataifa.

"Hakuna muda mwingine wa kufanya maandalizi zaidi ya huu tuliopata, kama mwalimu jukumu langu ni kuhakikisha natengeneza timu imara itakayojumuisha wachezaji wapya na wale wa zamani," amesema

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
9h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
9h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
12h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’