Wachezaji wanne wa Simba walioachwa jijini Dar es salaam kutokana na matatizo ya pasi zao za kusafiria, wametua Afrika Kusini na kushiriki mazoezi ya jioni ya kikosi cha Simba leo baada ya tatizo lao kupatiwa ufumbuzi
Mshambuliaji Meddie Kagere na kiungo Francis Kahata ni miongoni kwa wachezaji waliowasili Afrika Kusini leo
Wengine ni Deo Kanda na Sharaf Shiboub
Baada ya kuwasili wachezaji hao, kikosi cha Simba sasa kimekamilika kikiendelea na mazoezi chini ya kocha Mkuu Patrick Aussems




ADVERTISE HERE