Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wamefanikiwa kupata vibali vya kufanya kazi nchini kwa wachezaji wao sita wa kigeni
Simba ambayo kwa sasa iko kambini Rusteburg, Afrika Kusini, ilikamilisha usajili wa wachezaji wapya sita wa kigeni ambao watashiriki michuano mbalimbali na timu hiyo msimu ujao
Wachezaji ambao wamepata vibali ni pamoja na Wabrazil watatu, Wilker Henrique Da Silva, Gerson Fraga Vieira na Tairon Santos Da Silva
Wengine ni Deo Kanda kutoka DR Congo, Francis Kahata kutoka Kenya na Sharaf Shiboub kutoka Sudani
Aidha Simba pia imehuisha mikataba ya wachezaji wake watatu wa kigeni ambao ni Clatus Chama, Paschal Wawa na Meddie Kagere
ADVERTISE HERE