Huku Manula, kule Beno kazi wanayo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Jul 2019
Huku Manula, kule Beno kazi wanayo

Walinda lango wa Simba Aishi Manula na Beno Kakolanya wameendelea kujifua nchini Afrika Kusini katika maandalizi ya msimu mpya

Moja ya maeneo ambayo Simba haitakuwa na wasiwasi kabisa msimu ujao ni eneo la ulinzi wa lango

Misimu miwili iliyopita Simba ilimtegemea zaidi Manula ambaye alilazimika kucheza mechi nyingi bila ya kupumzishwa

Hata hivyo msimu ujao benchi la ufundi litakuwa na kazi ya kuamua nani akae langoni kutokana na ubora wa walinda lango hao

Beno aliyetua Simba akitokea klabu ya Yanga, alikuwa kipa namba moja wa timu hiyo kabla ya kufanya mgomo kushinikiza alipwe stahili zake

Beno aliibeba Yanga kwenye michezo mingi ukiwemo mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Simba ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana yeye akiibuka shujaa wa mchezo

Aidha kutokana na ushiriki wa Simba kwenye michuano mingi, msimu ujao huenda walinda lango hao wakapewa majukumu kufuatana na mashindano yaliyopo

Simba itashiriki Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa, Kombe la FA, kombe la Mapinduzi bila ya kusahau michuano ya Sportpesa Cup

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’