Aussems afurahishwa na muitikio wa wachezaji Afrika Kusini

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Jul 2019
Aussems afurahishwa na muitikio wa wachezaji Afrika Kusini

Kikosi cha Simba leo kimeingia siku ya tatu Afrika Kusini kikijifua kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara, ligi ya mabingwa na michuano mingine

Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Patrick Aussems ameeleza kufurahishwa na muitikio wa wachezaji wake katika mazoezi anayoendelea kuwapatia

Aidha amesema amefurahishwa zaidi na wachezaji wake wapya ambao wameonekana kuufahamu kwa haraka mfumo wa uchezaji unoutumiwa na Simba

"Bado tuna siku chache huku tangu timu imefika hapa, lakini naona juhudi za wachezaji wangu kwenye mazoezi ninayotoa, hii ni dalili nzuri kwetu," amesema Aussems.

Mbelgiji huyo amesema ataandaa programu maalumu kwa ajili ya kuhakikisha wachezaji wake wote wanafahamu vitu vya msingi, kabla ya baadhi ya nyota wake kurejea nchini

cut

Baadhi ya wachezaji wanapaswa kujiunga na kambi ya Timu ya Taifa kwa ajili ya maandalizi ya kuwavaa Kenya katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN).

Kambi ya timu ya Taifa itaanza Julai 21 ambapo nyota saba wa Simba watalazimika kurejea nchini kwa ajili ya maandalizi ya michezo miwili dhidi ya Kenya ambayo itapigwa JUlai 28 na August 04

Wachezaji wa Simba walioitwa timu ya Taifa ni Aishi Manula, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassani Dilunga, Ibrahim Ajib na John Bocco

Wachezaji hao wote walisafiri na timu Afrika Kusini

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’