Simba ilivyombana Mzee Kilomoni

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Jul 2019
Simba ilivyombana Mzee Kilomoni

Kile kiburi cha Mzee Hamisi Kilomoni kwa klabu ya Simba ni kama kimefikia tamati baada ya uongozi wa klabu hiyo kuonyesha uthibitisho kuwa mkataba wake ulikoma mwaka 2017 na sasa yeye sio mdhamini wa Simba

Juzi wakati akiongea na waandishi wa habari, Mtendaji wa Simba Crescentius Magori alionyesha nyaraka zilizotoka kwa kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali kwenda kwa wakili wa Mzee Kilomoni pamoja na barua ya Mahakama kwenda kwa wakili huyo zinazothibitisha kuwa Mzee Kilomoni siyo mdhamini tena wa Simba

Aidha Simba iko mbioni kupatiwa hati nyingine na Serikali ambapo mchakato huo ukikamilika hati alizonazo Mzee Kilomoni zitabaki kama kumbukumbu tu kwani hazitakuwa na maana yoyote

Hapo ndipo Simba itaweza kukamilisha mchakato wake wa mabadiliko kwa kukidhi matakwa ya Mwekezaji Mohammed Dewji 'Mo' ambaye anasubiri kupatiwa nyaraka hizo ili atoe fedha Bilioni 20 za uwekezaji

Kwa sasa Mzee Kilomoni anatapatapa tu. Jumatano ijayo ameitwa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Maadili ya TFF baada ya uongozi wa Simba kumshitaki kwa kuivuruga klabu hiyo

Huko anaweza kukumbana na kifungo cha kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu maisha yake yote!

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’