CAF yafuta mfumo wa michezo miwili ya fainali, ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Jul 2019
CAF yafuta mfumo wa michezo miwili ya fainali, ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho

Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) limefanya mabadiliko kwa michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho ambapo kuanzia msimu ujao mchezo wa fainali utakuwa mmoja tu

Kwa miaka mingi mfumo uliotumika ni michezo miwili ya fainali ambayo hupigwa nyumbani na ugenini

Rais wa CAF Ahmad Ahmada amesema uamuzi huo umepitishwa leo kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika Cairo, Misri

"Uamuzi mkubwa umechukuliwa na kamati ya utendaji ya CAF leo. Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika kuanzia sasa zitachezwa mechi moja," ameandika Ahmad kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter

Aidha tukio la kuvunjika kwa mchezo wa pili wa fainali ya ligi ya mabingwa mwaka huu kati ya Esperance dhidi ya Wydad Athletic linatajwa kuwa sababu ya kufikiwa uamuzi huo

Mchezo huo ulivunjika baada ya Wydad kugoma wakipinga maamuzi ya kunyimwa bao

Hata hivyo mwamuzi alishindwa kuthibitisha malalamiko hayo kwa kuwa mfumo wa VAR haukuwa ukifanya

Kulikuwa na dalili kuwa wenyeji Esperance walihusika kukwamisha mfumo huo ambao uliwabeba kwenye mchezo wa kwanza

Baadae CAF ilifuta matokeo ya mchezo huo na kuamuru urudiwe kwenye uwanja huru

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
48m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’