Beki mpya wa Simba Gerson Fraga ameeleza furaha yake kutokana na mapokezi aliyopata kwa mashabiki wa Simba
Fraga ni mmoja wa wachezaji watatu raia wa Brazil ambao wamesajiliwa na Simba
Wegine ni mshambuliaji Wilker Henrique da Silva na beki Tairone Santos da Silva
Fraga ambaye yuko Afrika Kusini kwenye kambi Simba, amesema kwa muda mfupi ambao amekaa nchini ametambua kuwa mashabiki wa Simba ni wakarimu na wanaipenda sana timu yao
"Nimefurahi kwa mapokezi na upendo ninaopata kutoka kwa mashabiki wa Simba," amesema
"Nina kazi ya kuhakikisha natoa mchango mkubwa kwa timu yangu ili kufikia malengo yaliyowekwa"
Akizungumzia kambi ya Afrika Kusini, Fraga amesema anaamini baada ya kambi hiyo watarejea wakiwa imara na bora
Simba itarejea jijini Dar es salaam baada ya wiki tatu tayari kwa Tamasha la Simba Day litakalofanyika August 08
Aidha baada ya mchezo huo, August 17 itaumana na Azam Fc kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii
August 23 itafungua pazia la ligi kuu ya Tanzania Bara kwa kuumana na JKT Tanzania kwenye mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru