Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kiliwasili salama Afrika Kusini jana na kuanza mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya
Hata hivyo baadhi ya nyota walishindwa kusafiri jana kutokana na hati zao za kusafiria kutokamilika
Mfungaji bora wa ligi kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita, Meddie Kagere ni miongoni mwa wachezaji ambao wamebaki jijini Dar es salaam
Wengine ni nyota wapya kiungo Francis Kahata na mshambuliaji Deo Kanda
Uongozi wa Simba umesema wachezaji hao wataungana na wenzao siku chache zijazo kwani wako katika hatua za mwisho kukamilisha Visa zao
ADVERTISE HERE